MAENEO YOTE YA JIJI LA MWANZA NA VIUNGA VYAKE KUKOSA MAJI



TAARIFA KWA UMMA

UKOSEFU WA MAJI MAENEO YOTE YA JIJI LA MWANZA NA VIUNGA VYAKE

Tumepokea taarifa kutoka TANESCO, kuwa Tarehe 16 Februari, 2019 kuanzia Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 11:00 Jioni watazima umeme kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo eneo la Chanzo cha Maji Capri-Point.

Kufuatia taarifa hiyo, tunasikitika kuwataarifu wateja wetu wote kuwa hakutakuwa na uzalishaji wa maji hadi hapo huduma ya nishati ya umeme itakaporejea katika hali yake ya kawaida.

Tunawashauri kutunza maji yatakayotosha katika kipindi hicho ambacho kutakuwa hakuna uzalishaji wa maji. 

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia kituo chetu cha huduma kwa mteja kwa namba 0800110023 (Bure).

Imetolewa Tarehe 15 Februari, 2019 na: -

OFISI YA UHUSIANO

MWAUWASA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527