MCHINA 'MALKIA WA MENO YA TEMBO' ATUPWA JELA MIAKA 17 TANZANIA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kifungo cha miaka 17 jela washtakiwa watatu akiwemo raia wa China, Yang Feng Glan (66) maarufu Malkia wa Tembo.

Kila mmoja atatumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh13bilioni.

Mbali na Glan, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 21/2014 ni Salvius Matembo na Philemon Manase.

Hukumu hiyo umetolewa leo mchana Februari 19, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi baada ya kuwatia hatiani washtakiwa hao.


Na Hadija Jumanne, Mwananchi 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527