RAIS MAGUFULI ATEMBELEA OFISI ZA AFRICAN MEDIA GROUP WAMILIKI WA CHANNEL 10 NA MAGIC FM,ASEMA NI MALI YA CCM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh. Dkt John Pombe Magufuli Magufuli leo ametembelea kituo cha televisheni cha channeli ten ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 42 ya chama cha Mapinduzi ambacho Rais ndio mwenyekiti wa chama hicho.

Amesema kutokana na Uhitaji wa vifaa vya kisasa kama Kamera za kisasa, Rais ameahidi kuwachangia milioni Mia Moja kwa ajili ya ununuzi wa kamera hizo, na atawatafutia milioni zingine 100 ili zitumike katika maboresho ya kituo hicho.

Aidha amewathibitishia kuwa hakuna mfanyakazi atakayefukuzwa kwa sababu ya itikadi zake na ameahidi kuwatafutia jengo la CCM lenye hadhi nzuri ili waweze kuhamishia ofisi za kituo hicho. 

"Nimefika hapa leo ili niwaambie African Media Group ni mali ya CCM.Hakuna atakayefukuzwa kazi no matter wewe ni muumini wa chama gani" 

"Ili kuboresha kazi yenu, tutanunua vifaa vipya ili muweze kuwafikia watu wengi sana.Sikujua Channel 10 na Magic FM zinatokea kwenye jengo la ajabu kiasi hiki.

"Tutasaidiana kufanya utafiti wa majengo ya CCM ili tuangalie wapi tunaweza kuweka ofisi za vituo hivi.Hata mkitaka jengo la Ofisi ya Mwenyekiti wa CCM, Mimi nitakubali.Hata jengo la kupanga tutatafuta, ofisi nyingi zimehamia Dodoma.

Kadhalika amesisitiza kwamba vyombo vya habari vipo huru katika utendaji wake lakini amewaasa kuzingatia Sheria, kanuni, taratibu na tamaduni za Nchi ili kusaidia Nchi katika kulinda amani na utulivu na kukuza uchumi ambao utawanufaisha Watanzania.


"Vyombo vya habari vinatakuwa kuwa free vizungumze, Tanazania freedom of expression ipo‬.‪Ndio maana kuna vyombo vya habari vilivyosajiliwa zaidi ya 170 na zaidi‬.Tuzingatie mipaka ya uandishi, maadili ya nchi yetu, tabia za jamii zetu na Katiba yetu‬.‪Kwamba hili linaweza kuzungumzwa hapa, hili linafaa huku au hili linafaa kwenye vikao‬"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527