OFISA TAKUKURU MATATANI KWA TUHUMA YA KUMBAKA MTOTO WA DADA YAKE

Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Rukwa, Jonas Jackson (34) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka na kisha kumlawiti mtoto wa dada yake aliyekuwa akiishi naye.

Ofisa huyo alikamatwa Februari 7, 2019 baada ya mtoto huyo kwenda kuripoti kituo kikuu cha polisi mjini Sumbawanga kufuatia kuchoka kufanyiwa vitendo hivyo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa jana Jumatatu Februari 11, 2019 baada ya mlalamikaji mwenye umri miaka 18, kwenda polisi kutoa taarifa ya vitendo vya unyanyasaji anavyofanyiwa.

Msichana huyo amedai amekuwa akifanyiwa vitendo hivyo na mjomba wake tangu Septemba, 2018.

Amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo mara kwa mara anapotoka kwenye starehe zake na kurejea nyumbani akiwa amekunywa pombe alikuwa na tabia ya kumnywesha pombe, kuanza kumbaka na kumwingilia kinyume na maumbile.

Kamanda Kyando amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi na muda wowote atafikishwa mahakamani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527