AMUUA MWANAFUNZI KWA KUMCHINJA NA SIME KISA PETE

Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kereto Likoko [Mmasai] kwa madai ya kumuua Mwanafunzi Samson Conradi anayesoma katika Chuo cha Faraja kwa kumkata na sime shingoni kwa madai ya kushindwa kumlipa fedha ya pete ambayo alikuwa akiuza.

Akizungumza jana Jumatatu Februari 11, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Isah amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa kabla ya kifo marehemu akiwa na mwanafunzi mwenzake, Andrew Charles, walikuwa katika mazungumzo ya kuuziwa pete na mtuhumiwa huyo.

“Wakati wakiendelea na mazungumzo hawakuelewana na mtuhumiwa akitaka kupatiwa fedha yake, na alichomoa sime na kumjeruhi marehemu shingoni. Alivuja damu nyingi na amefariki dunia,”amesema Kamanda Issah

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527