MENEJA MAWASILIANO TFS AFARIKI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI


Hakuna ajuaye siku wala saa. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya meneja mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Glory Mziray kufariki dunia leo mchana Jumanne Februari 19, 2019.

Glory amefikwa na umauti wakati akizungumza na waandishi wa habari. 

Hali yake ilibadilika ghafla muda mfupi baada ya kumaliza kusoma taarifa ya TFS kuhusu upandishaji hadhi wa misitu.

Inaelezwa kuwa meneja huyo alizungumza kwa uchangamfu na alipomaliza alionekana kama kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu.

Alikimbizwa katika kituo cha Afya TMJ kilichopo Chang’ombe kwa ajili ya matibabu.

Baada ya kumfanyia uchunguzi madaktari wakaeleza kuwa Glory amefariki dunia kabla ya kufikishwa hospitalini hapo.
Mtendaji Mkuu  wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake Glory Water Mziray aliyekuwa  Meneja Habari na Mawasiliano kilichotoke leo Jumanne 19 Februari 2019 mchana mara baada ya kujisikia vibaya akiwa anatekeleza majukumu yake kwa kuongea na waandishi wa habari ofisini na kukimbizwa katika Hospitali ya TMJ Temeke ambapo madaktari walithibitisha kuwa amefariki dunia. Mipango ya Mazishi inafanywa.

Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake  lihimidiwe amen!

Imetolewa na 
Utawala- TFS Makao Makuu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post