Picha : VIJANA WA KANISA LA LIVING WATER CENTER KAWE WACHANGIA DAMU DAR

Vijana wa Kanisa la Living Water Center Kawe chini ya Apostle Onesmo Ndegi na Apostle Lilian Ndegi lililopo katika Manispaa ya Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam wameshiriki katika zoezi la kuchangia damu  katika kilele cha wiki ya vijana kanisani 
hapo. 

Vijana hao waliamua  kushiriki katika zoezi hilo siku ya Jumapili ikiwa ni katika kuunga mkono juhudi mpango wa Taifa wa Damu Salama chini ya Wizara ya Afya  wa kutoa damu ili kuokoa uhai wa wahitaji wa damu katika hospitali  nchini. 

Akiongoza zoezi la uchangiaji damu Mchungaji wa Vijana Kanisani hapo ,Albert Monyo aliwataka vijana katika jamii kuwa na moyo wa kutoa damu  ili kuwasaidia wenye uhitaji maana kwa kufanya hivyo kunasaidia  kupunguza uhitaji mkubwa wa damu uliopo kwenye hospitali nyingi hapa nchini.

Naye Afisa muhamasishaji Damu Salama kanda ya Mashariki Mariam Juma  alitoa rai kwa waamini wa madhehebu mbalimbali na wanajamii kwa ujumla  kujenga tabia ya kuwa wanachangia damu mara kwa mara bila kusubiri dharula. 

Alisema uhitaji wa damu bado ni mkubwa na Ofisi  ya Damu Salama bado hijawahi kuziba pengo la upatikanaji wa damu ya  kutosha kwa asilimia mia moja.
Vijana wakitolewa damu 

Baadhi ya Vijana wachangiaji damu  wakimsikiliza Afisa Mshauri kutoka Damu Salama katika majadiliano kabla ya
kutoa damu
Albert Monyo Mchungaji wa Vijana kanisani hapo akimsikiliza Afisa Mshauri kutoka Damu Salama katika majadiliano kabla ya kutoa damu.
Albert Monyo Mchungaji wa Vijana Kanisani hapo alipowaongoza vijana katika zoezi la uchangiaji damu

Afisa mshauri kutoka damu salama akimshauri mmoja wa wachangiaji damu katika zoezi hilo 
Mmoja wa wachangiaji wa damu akionesha kadi yake ya wachangiaji mara kwa mara 
Mmoja wa wachangiaji wa damu akioesha kadi yake ya wachangiaji mara kwa mara 
Maafisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama walioendesha zoezi hilo. 
Maafisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama walioendesha zoezi hilo 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post