DIWANI WA CHADEMA AWEKWA NDANI KWA AMRI YA RC KISA DHARAU KAKUNJA NNE KWENYE KIKAO


 Diwani wa Susuni (Chadema), Abiud Solomon amesimulia jinsi alivyoondolewa kwenye kikao na mkuu wa mkoa wa Mara, Adam Malima na kuwekwa ndani kwa saa saba kisha kuachiwa akielezwa kuwa ana dharau kwa kuwa alikunja nne kikaoni.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Februari 2, 2019 amesema Malima alitoa agizo hilo kwa polisi kumweka ndani kwa madai kuwa ameonyesha dharau kwenye kikao cha kumtambulisha mkuu mpya wa wilaya ya Tarime, Charles Kabeho.

Katika tukio hilo lililotokea jana Ijumaa Februari Mosi, 2019, Solomon amesema kabla ya kuondolewa alihojiwa kuhusu wadhifa wake, “lakini nilishangaa kusikia agizo la kuniweka ndani kisa nimekunja nne kwenye kikao cha mkuu wa mkoa.”

“Niliwekwa ndani kuanzia saa saa 9 alasiri hadi saa 3 usiku baada ya viongozi wangu wa chama kufanya taratibu za kuniwekea dhamana wakafanikiwa kunitoa lakini nikatakiwa kurudi siku ya Jumatatu Februari 4.”

Ameongeza, “Tulikuwa na kikao cha kumkaribisha mkuu wa wilaya mpya, nilipata nafasi ya kukaa eneo la waandishi wa habari ili kuwapisha wapite, nililazimika kubebanisha miguu yangu (kukunja nne) ili kutoa nafasi ya wao kupita na kufanya kazi yao vizuri, ila ikachukuliwa kwamba namdharau mkuu wa mkoa.”
Via Mwananchi

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527