Saturday, February 16, 2019

ALICHOKISEMA WAZIRI LUGOLA BAADA YA KUFIKA KABURINI KWA KIJANA ALIYEPIGWA RISASI KITUO CHA POLISI

  Malunde       Saturday, February 16, 2019
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amefika nyumbani kwa kijana Richard Peter, ambaye amefariki siku za hivi karibuni kwa kupigwa risasi akiwa katika kituo cha polisi.

Akizungumza mbele ya familia hiyo ambapo alifika kwa ajili ya kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa Magufuli, Lugola amesema polisi linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani.

Lugola amesema; “ Rais alipopata taarifa zilimshtua na sababu moja kubwa ya kumshtua ni kwamba amefia kwenye eneo la polisi, kwa hiyo amenituma niwapeni pole sana”

"Niwaombe watanzania mliamini jeshi la polisi maana si jehi la kuua watu na wala hatufundishi askari wetu kuua watu kwa hiyo isitafsiriwe jeshi letu ni la kuua watu muwe nasubira" .Ameongeza Kangi Lugola.

Waziri huyo kwa sasa yuko ziarani Mkoa wa Arusha ambapo siku ya kwanza alizungumzia kuhusiana na tukio la kushambuliwa na Tundu Lissu pamoja na kuzungumza na madereva wa bodaboda mapema jana.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post