ZITTO KABWE : WABUNGE WAPENDA SIFA WANATUKWAMISHA BUNGENI


Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ameeleza kuwa wingi wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) bungeni kuna kwamisha maslahi ya wananchi kutokana kutumia wingi wao kupitisha yanayowapendeza watawala.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Ofisi za Chama cha CHAUMA akiambatana na viongozi wa vyama kumi vya upinzani vilivyoungana kutetea demokrasia na kupinga muswada wa sharia ya vyama vya siasa.

Vyama hivyo ni pamoja na ACT-Wazalendo, Chama cha Wananchi (CUF) Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi, NRD, CCK, CHAUMA.

Zitto amesema kuwa muswada wa sheria ya vyombo vya habari utapelekwa bungeni ambapo wabunge wa CCM ambao ndiyo wengi bunge watawashinda wabunge wachache wa upinzani na kupelekea kupita kwa sheria hiyo ya vyama vya siasa ambayo wanaiona ni sheria shetani na ovu kwa demokrasia.

“Bunge limejaa wabunge wa CCM, kuna wabunge wazuri wa chama cha mapinduzi lakini kuna wabunge ‘makasuku’ kiasi kwamba muswada huu ukienda utatoka mbaya zaidi,” amesema Zitto na kuongeza.

“Kuna wabunge wapenda sifa wataufanya muswada huu kuwa mbaya zaidi na tayari tuansikia wapo wabunge watakaopendekeza kwenye sharia hiyo kwamba hakuna kufanya mikutano mpaka uchaguzi hadi uchaguzi.”

Zitto ameeleza kuwa muswada huo uliolenga kuua demokrasia ya kweli ambapo Msajili wa vyama vya siasa atakuwa na mamlaka kamili juu kuingilia mambo ya ndani ya vyama vya siasa.

Via Mwanahalisionline

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527