Kocha huyo ambaye timu yake inaongoza ligi ikiwa na alama 50, ameweka wazi kuwa kwasasa haoni timu nyingine ya kushindana nayo kwenye mbio za ubingwa zaidi ya Simba na Azam.
''Timu zinazoshika nafasi ya 4 na 5 tumezipita takribani alama 17 na ili zishindanie ubingwa na sisi ni lazima zishinde mechi zake zote huku sisi tukifungwa mechi 5. Kwahiyo ni ngumu ila zinaweza kutufunga lakini sio kutufikia kwenye mbio za ubingwa'', amesema.
Aidha Mwinyi Zahera amekiri kuwa Simba ina viporo vitano ambavyo ikishinda mechi zote itakuwa na alama 45 hivyo kuzidiwa alama 5 na Yanga yenye alama 50 huku Azam yenye alama 40 na kiporo kimoja inaweza kufikisha alama 43 na kuzidiwa 7 lakini kutokana na wingi wa mechi zilizobaki wanayo nafasi ya kushindania ubingwa.
Mechi za Yanga, Azam FC na Simba SC kwenye ligi kuu zimesimama kwasasa kutokana na timu hizo kuwa kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup Visiwani Zanzibar ambayo yameanza jana Januari 1, 2019 na yanatarajiwa kumalizika Januari 13.
Chanzo-Eatv