HAWA NDIYO WAAMUZI MCHEZO WA SIMBA NA JS SAOURA


Wachezaji wa Simba na JS Saoura

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza waamuzi watakaochezesha mechi ya Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba na JS Saoura. 

Waamuzi hao ni Joshua Bondo ambaye atasimama kama mwamuzi wa kati, waamuzi wasaidizi Oamogetse Godisamang, Moemedi Godfrey Monakwane na mwamuzi wa akiba, Kutlwano Leso, wote kutoka nchini Botswana.

Kamishna wa mechi ni James Leonard Mwenda kutoka nchini Malawi, msimamizi mkuu wa mchezo huo ni Alexander Sakyi Asante kutoka nchini Ghana.

Simba itawakaribisha JS Saoura katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi ambao utapigwa Januari 12 Jijini Dar es salaam.

Ikumbukwe Simba ipo katika kundi D pamoja na vigogo wawili ambao ni Al Ahly ya Misri na AS Vita Club ya Congo DRC pamoja na JS Saoura ya Algeria ambayo haina uzoefu mkubwa katika michuano hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post