VYAMA VYA SIASA VYAALIKWA KUTOA MAONI MUSWADA WA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA

Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria inatarajia kukutana na wawakilishi wa vyama vya siasa Januari 19 na 20, 2019 kuwasikiliza na kupokea maoni yao kuhusu muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018.


Kamati hiyo itapokea maoni yao baada ya kumaliza vikao vyake na wadau wengine vitakavyofanyika Januari 17 na 18, 2019 mjini Dodoma kuhusu muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2018 na kufuatiwa na mkutano wake na wawakilishi wa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu hapa nchini ambao wanapinga muswada huo.


Bunge litapokea maoni hayo wakati leo kesi iliyofunguliwa kupinga Bunge kujadili muswada huo ikiwa inatolewa uamuzi mahakamani.


Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu na wanasiasa watatu ambao ni kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, Joram Bashange na Salim Bimani kutoka Chama cha Wananchi (CUF) kwa niaba ya wanachama wa vyama 10 vya siasa dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post