Baada ya mechi ya AS Vita vs Simba kumalizika, kocha msaidizi wa Vita, Raoul Shungu ambaye aliwahi kufundisha Yanga.
Amezungumzia mchezo wao dhidi ya Simba, na alisema waliangalia mechi kadhaa za Simba na kubaini mapungufu ambayo wameyatumia na kupata ushindi.
“Simba ni timu nzuri lakini wanacheza mpira ambao sio wa kasi, wanapiga pasi ambazo kwenye mashindano hazina faida, wanapoteza muda mwingi kupiga pasi za hapa na pale badala ya kwenda mbele kutafuta nafasi. Sisi tunarudi nyuma tukipata mpira tunacheza kwa speed.”
Shungu amesema katika kipindi chote alichofundiaha Yanga, alishinda mechi zote alizokutana na Simba.