MUONEKANO WA JENGO LA TAMISEMI UTAKAVYOKUWA

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imekuja na maajabu mpya kwa kujenga Jengo la Kisasa litakalokuwa na mvuto wa kipekee katika mji mpya wa Serikali Jijini Dodoma.

Ujenzi huo unatekelezwa kwa kutumia utaratibu wa manunuzi ya moja kwa moja ‘Force Account’ na utagharimu Sh.Bilioni moja ambazo zimetolewa na Rais Dk.John Magufuli kwa kila Wizara.

Jengo hilo litachukua watumishi zaidi ya tisini pamoja na kumbi mbili za mikutano ikilinganishwa na majengo mengine yatakayochukua watumishi chini ya arobaini.


Kupitia utaratibu huo kuna kamati nne za ushindi zimeundwa ili kufanikisha ujenzi ambazo ni Kamati ya Manunuzi, Kamati ya Vifaa, Kamati ya Ujenzi, na Kamati ya Usimamizi na ufuatiliaji.


Katika kufanikisha ujenzi huo, TAMISEMI inatumia kitengo cha Ujenzi cha Chuo Kikuu Mbeya kama fundi wa ujenzi huo chini ya Wakala wa Majengo(TBA) kama mshauri.


Aidha, kamati ya ujenzi ya TAMISEMI iliyo sheheni wahandisi wake kutoka makao makuu wanasimamia kila kipande cha ujenzi huo ili kuendana sambamba na ushauri wote unaotolewa na TBA kwa lengo la kupata jengo bora zaidi.


Katika kufanikisha mapinduzi hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo alitoa maelekezo mahususi kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ambayo ni Taasisi iliyo chini ya usimamizi wa Ofisi ya TAMISEMI kuhakikisha unajenga jengo la aina hiyo pia kwa kutumia fedha za ujenzi walizonazo kwasasa.


Amesema hataki kuona Taasisi hiyo inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kupanga jengo na kwamba ifikapo Julai mwaka huu, agizo ambalo TARURA wameanza utekelezaji wake.


Kasi ya ujenzi wa jengo hilo inawapa changamoto Wakuu wa Mikoa, Wilaya, na Wakurugenzi wa Halmashauri hapa ambao wamepewa fedha za ujenzi wa ofisi lakini bado wanasuasua. Hili ni jambo la kutafakarisha kwa viongozi wote wa Mikoa, Wilaya, na Halmashauri zote nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527