RAIS MAGUFULI AAGIZA TAASIS ZOTE ZA KIFEDHA ZIUNGANISHWE



Rais Dk John Magufuli ameigiza Wizara ya Fedha na Mpango kuunganisha taasis za kifedha ziwe chini ya mfumo mmoja wa kimawasiliano utakaoirahishia Serikali kujua mapato yanayokusanywa lakini pia kupunguza gharama za uendeshaji wa kila taasisi.

Ametoa agizo hilo leo Ijumaa Januari 18, alipokuwa akihutubia viongozi mbalimbali na wananchi waliojitokeza katika Makabidhiano ya mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu (TTMS) nchini, uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema mfumo huo utarahisisha taasis hizo hasa ya ukusanyaji mapato kwani taarifa zitakuwa za uwazi hivyo itapunguza udanganyifu na ubadhirifu wa fedha unaofanywa na baadhi ya watumishi wasio wazalendo.

“Naiagiza Wizara ya Fedha kuhakikisha taasisi zote za kukusanya mapato na za kifedha ziunganishwe na mfumo mmoja wa kieletroniki utakaowasaidia kufanya kazi zao kisasa zaidi.

“Nitashangaa kama hazitaungaishwa mtafanya niamini mnafanya kazi gizani na mimi nataka tuwe na tochi ya kuwamulika na tochi hiyo ni kuwa na mfumo unganishi,” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema bila mfumo huo serikali ingeendelea kupoteza fedha nyingi bila kujua kwani wanaotakiwa watote taarifa za ukusanyaji mapato wangeleta kile wanachokitaka wao bila mtu mwingine kujua lakini sasa taarifa zote zitakuwa wazi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post