Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe akikagua sehemu ya kingo za daraja la Dumila, ambalo hivi karibuni kingo za daraja hilo ziliathirika kutokana na mvua zilizonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Kamati ya Usimamizi wa maafa ya mkoa na wilaya zilichukua hatua ya kurejesha hali ya kawaida ya daraja hilo kwa wakati.
Muonekano wa mawe yaliyowekwa katika Daraja la Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro, ikiwa ni hatua ya kamati ya Usimamizi wa maafa ya mkoa na wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro ya kurejesha hali ya kawaida ya daraja hilo kuweza kupitika. Daraja hilo liliathirika kingo zake kutokana na mvua zilizonyesha wilayani Kilosa juzi.
Vyombo vya Usafiri, ikiwa ni magari, pikipiki na baiskeli pamoja na watembea kwa miguu wakipita katika Daraja la Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro, baada ya kingo za daraja hilo zilizo kuwa zimeathiriwa na mvua kujengwa kutokana na mvua zilizonyesha wilayani Kilosa juzi. Hatua hiyo ilifanywa kwa wakati na kamati ya Usimamizi wa maafa ya mkoa na wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro .
Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe akimsikiliza Mratibu wa Kurejesha Hali Daraja la Dumila, Mhandisi wa TANRODS- Morogoro, Deogratius, akimueleza hatua walizochukua katika kurejesha hali ya hilo ambalo hivi karibuni kingo za daraja hilo ziliathirika kutokana na mvua zilizonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro. Kamati ya Usimamizi wa maafa ya mkoa na wilaya zilichukua hatua ya kurejesha hali ya kawaida ya daraja hilo kwa wakati.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)