Monday, January 7, 2019

MGOMBEA UBUNGE UKAWA JIMBO LA KWIMBA AKABIDHI BUSARA TANO KWA KATIBU MKUU CCM

  Malunde       Monday, January 7, 2019

Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) amejiunga na Chama Cha Mapinduzi CCM na kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally.

Otto amejiunga CCM leo Jumatatu Januari 7,2019 wakati wa mkutano wa Katibu huyo wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi kadi ya CUF na busara tano za kustawisha Chama Cha MapInduzi,Otto alisema ameamua kujiunga CCM kwa sababu ni chama chenye mipango kazi inayotekelezwa kwa vitendo na uaminifu kama Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015. 

“Nimeamua kujiunga CCM kwa sababu ya utashi nilionao wa kutumikia wananchi kupitia siasa na kuamini kwamba CCM ndiyo mahali pekee penye ndoto na dira ya utekelezaji wa sera ili kuwaletea maendeleo wananchi”,alisema Otto. 

“Mheshimiwa Katibu Mkuu,naomba kukukabidhi bango langu nililolitumia wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 nikiwania ubunge jimbo la Kwimba lakini pia naomba kukukabidhi karatasi hii yenye busara tano zinazolenga kukistawisha Chama Cha Mapinduzi”,aliongeza. 

Akiwa katika mkutano huo,Katibu Mkuu wa CCM ,Dkt. Bashiru Ally amepokea wanachama 126 wapya wakiwemo kutoka vyama vya upinzani.


Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) akizungumza wakati wa kujiunga CCM leo -Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog


Katibu mkuu CCM ,Dkt. Bashiru Ally akiwa ameshikilia bango la Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA).Kulia ni Ntiga Julius Otto akiwa ameshikilia karatasi yenye busara tano za kustawisha Chama Cha Mapinduzi aliyoikabidhi kwa Dkt. Bashiru.
Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) akishikana mkono na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally akimkaribisha CCM.
Mgombea ubunge jimbo la Kwimba mkoani Mwanza mwaka 2015 ,Ntiga Julius Otto kupitia Chama Cha Wananchi CUF (UKAWA) akiwa amekaa na makada wenzake wa CCM katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post