Gabriel Nyantori (25) amefikishwa mbele ya mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Serengeti mkoani Mara akituhumiwa kwa makosa ya kuzini na dada yake na kumpa mimba.
Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile, mwendesha mashitaka, Faru Mayengela leo Jumatatu Januari 14, 2019 amesema mshitakiwa anakabiliwa na makosa mawili.
Amesema kosa la kwanza ni kuzini na dada yake mwenye umri wa miaka (16) mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Kibeyo na kosa la pili ni kumpa mimba dada yake, makosa ambayo aliyatenda Aprili 30, 2018 nyumbani kwao, Kibeyo.
Na Anthony Mayunga, Mwananchi