Wabunge Uingereza wanajitayarisha kupiga kura kwa iwapo kuunga au kutounga mkono mpango wa Theresa May wa kujitoa katika Umoja wa Ulaya.
Kura hiyo inayotajwa kuwa Kura yenye umuhimu itafanyika baadaye leo wakati mjadala wa siku tano kuhusu Brexit ukikamilika.
Bi May amewataka wanasiasa kuunga mkono mpango wake au kuhatarisha kuwavunja moyo raia wa Uingereza.
Lakini huku wabunge wake mwenyewe wakitarajiwa kujiunga na wa vyama vya upinzani kupiga kura dhidi ya mpango huo, inatarajiwa pakubwa kwamba mpango huo hautofaulu.
Wabunge pia watapata fursa ya kutoa mapendekezo ya marekebisho ambayo yanaweza kuunda upya mpango huo kabla ya kura kuanza 19:00 kwa saa ya GMT.
Chanzo:Bbc