WANAFUNZI 10 BORA, SHULE 10 BORA, SHULE 10 ZA MWISHO MATOKEO KIDATO CHA NNE 2018. WA MATUSI WAMEFUTIWA

 Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) leo limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.29 kutoka asilimia 77.09 mwaka 2017 hadi asilimia 78.38.


Takwimu zinaonyesha idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa daraja la kwanza hadi tatu imeongezeka. Mwaka 2016 ilikuwa asilimia 27.60, mwaka 2017 asilimia 30.15, na mwaka 2018 ni asilimia 31.76.

Hope Mwaibanje ndiye mtahiniwa aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 yaliyotangazwa leo Januari 24, 2019 mjini Dodoma na katibu mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde.

Dk Msonde amesema Mwaibanje wa Shule ya Sekondari Ilboru ndiyo amekuwa kinara akifuatiwa na Avith Kibani wa Marian Boys ya mkoani Pwani.

Walioshika nafasi ya tatu hadi ya sita wote ni wa shule ya sekondari ya St Francis Girls ya mkoani Mbeya ambao ni Maria Manyama, Atughulile Mlimba, Flavia Nkongoki na Leticia Ulaya.

Mwanafunzi wa saba na wa nane kitaifa ni Gibson Katuma na Bryson Jandwa (wote wa Marian Boys ya mkoani Pwani).

Idegalda Kiluba wa St Francis Girls ameshika nafasi ya tisa kitaifa na Isack Julius wa Marian Boys ya Pwani ameshika nafasi ya 10.

Kwa matokeo hayo, kati ya watahiniwa 10 bora kitaifa, watahiniwa watano ni wa Shule ya Sekondari St Francis Girls, wanne wa Shule ya Marian Boys huku Mwaibanje akiwa pekee wa shule ya Serikali ya Ilboru.

Shule 10 zilizofanya vyema katika matokeo kitaifa ni St Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera), Marian Boys, Ahmes, Marian Girls (zote Pwani), Canossa, Bright Future Girls (zote Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa). 
Shule 10 za mwisho katika mtihani wa kidato cha nne 2018


Pwani Mchangani (Kaskazini Unguja),Ukutini (Kusini  Pemba),Kwediboma (Tanga), Rwemondo( Kagera),Namatula (Lindi), Kijini (Kaskazini Unguja),Komkalakala (Tanga), Kwizu (Kilimanjaro), Seuta (Tanga) na Masjid Qubah Muslim (Dar es salaam)
Wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari ya Malinyi mkoani Morogoro wamefutiwa matokeo hayo baada ya kubaini shule hiyo kuvujisha mtihani huo. Pia NECTA imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani, kutokana na udanganyifu huo na wahusika wote watachukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.

NECTA pia imebainisha kufuta matokeo ya wanafunzi walioandika matusi kwenye mitihani yao kitaifa ya kidato cha nne ambapo kati ya watahiniwa hao waliofutiwa matokeo, watahiniwa 71 walikuwa ni wa kujitegemea ambapo wawili walifutiwa kwa makosa ya kuandika matusi kwenye mtihani huo.


ANGALIA MATOKEO HAPA

Pakua App ya Malunde 1 blog tuwe tunakutumia habari zote moja kwa moja kwenye simu yako

Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyFDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post