MWANAFUNZI BORA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2018...TUMAINI LUTHERAN IMEFUTIWA MATOKEO

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, na kutaja shule 10 zilizofanya vyema katika mtihani huo kwa shule zenye watahiniwa zaidi ya 40.Wakati shule binafsi zikifanya vyema, mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi katika mtihani huo ni wa shule ya sekondari Ilboru ya Arusha, Hope Mwaibanje.

Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Januari 24, 2019 mkoani Dodoma katibu mkuu wa baraza hilo, Dk Charles Msonde amezitaja shule hizo kuwa ni St Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera), Marian Boys, Ahmes, Marian Girls (zote Pwani), Canossa, Bright Future Girls (zote Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa).

Katika matokeo hayo, watahiniwa 252 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na kati yao, 71 ni wa kujitegemea huku wawili kati yao wakiandika matusi.

Wakati huo huo (Necta) imefuta matokeo ya wanafunzi 57 wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari ya Malinyi mkoani Morogoro baada ya kubaini shule hiyo kuvujisha mtihani huo.

Mbali na kufuta matokeo hayo, Necta imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 24, 2019 na Katibu Mkuu mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde wakati akitangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018 mkoani Dodoma.

Amesema wameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527