MANARA APOZA MACHUNGU YA GOLI 5 KWA KUJIFANANISHA NA YANGA

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya timu yake kunyukwa goli 5-0 dhidi ya Klabu ya AS Vita ya DR Congo, kwenye mchezo wa klabu Bingwa barani Afrika .


Manara licha ya kukiri wazi timu yake kufungwa, kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa kipigo hicho kinamkumbusha miaka ya nyuma wakati Simba walivyowanyuka Yanga goli 5-0 kunako dimba la Taifa.

“Nani aliokwambia Simba ndio wa kwanza kufungwa Tano?hebu Gongowazi njooni hapa,lini tuliwafunga tano mara ya mwisho, au mwajitoa fahamu? Na vp kale kananiu nasikia Stand wamekinaniliu? Au bado kipo?,“ameandika Haji Manara .

Kufuatia matokeo ya mchezo huo, Simba inakuwa nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Kundi D, huku Al Ahly ikiongoza na ikifuatiwa na AS Vita na JS Saoura ikishika mkia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527