Picha : WATAFITI WATAKIWA KUONGEZA NGUVU KATIKA UTAFITI WA UGONJWA WA MALARIA


Mtaalamu wa magonjwa ya Damu, Vinasaba na Saratani Professa Lucio Luzatto wa Chuo cha MUHAS akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wageni waalikwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.
Wageni waalikwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa akiwasiliasha mada ya 'Malaria kwa akinamama wajawazito na Watoto' katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mtaalam wa Masuala ya Dawa wa Chuo cha MUHAS, Prof. Omary Minzi akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Wageni waalikwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Prof Andrew Barnabas Pembe akifuatilia kwa makini mada.
Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha MUHAS, Dkt Bill Ngasala akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu MUHAS wakifuatilia.
Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Damu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Julie Makani (kwanza kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya ugonjwa wa Siko Seli unavyoendana na ugonjwa wa Malaria.
Mtafiti wa Malaria wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu kilichopo Bombo Hospitali, Tanga, Deus Ishengoma akizungumzia ukata wa fedha unavyonyongonyesha tafiti bunifu.
Mmoja ya mdau wa masuala ya afya akiuliza swali.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma MUHAS na Mloganzila, Hellen Mtui akitoa shukrani zake za pekee kwa wote walioweza kushiriki katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Muhadhara huo, Prof. Lyamuya akihitimisha kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Utafiti umeonyesha ugonjwa wa Malaria kwa akinamama wajawazito na watoto umepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na awali.

Kwa upande wa Zanzibar ugonjwa wa Malaria umepungua kwa kiwango kikubwa hivyo ni vyema Tanzania Bara kuendelea kupambana ili ifikapo 2030  tatizo la ugonjwa wa Malaria kwa jamii umalizike.

Hayo ameyabainisha Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa anayesimamia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaaluma  wakati akiwasiliasha mada katika kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambalo Mada ilikuwa ni 'Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya malaria Tanzania' lililofanyika jijini leo Dar es Salaam.

Amesema kuwa kadili mama mjamzito anavyotumia vizuri dawa za kujikinga na ugonjwa wa  Malaria wakati akiwa amepata ujauzito ndivyo anavyoweza kuepukana na ugonjwa huo.

"Kawaida mama mjamzito anapofika wiki ya 13 huwa anapewa dawa za kuzuia Ugonjwa wa Malaria kwa ajili ya yeye na kumkimkinga mtoto, hivyo akizitumia sawa sawa kwa kufuata maelekezo ya dokta pindi anapojifungua huwa salama," amesema.

Prof Kamuhabwa amesema kuwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyofanyika katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam imeonyesha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria yamepungua chini ya asilimia moja jambo linaloletea faraja kubwa.

"Tafiti ni jukumu letu kubwa na tunaangalia magonjwa ya kipaumbele katika nchi na Malaria ni ugonjwa wa kipaumbe maana unaathiri akinamama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 5 hivyo hatuna budi kupambana zaidi" amesema.

Amesema kwa sasa MUHAS wanaendesha tafiti nyingine ya dawa mbadala ya Malaria kwa akinamama wajawazito na watoto maana dawa ile ya awali SP imeonyesha kuwaletea sugu akina mama.

"Tunafanya tafiti huko Rufiji ya dawa mbadala ya kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria ambapo Shirika la Afya Duniani limetutaka tufanyie utafiki katika nchi mbali mbali dunia japo wenzetu Kenya na Uganda matokeo yameonyesha dawa hiyo inafanya vizuri lakini kabla hapa kwetu hatujaanza kuitumia lazima nasi tufanye utafiki ila matokeo ya awali yanaonyesha dawa hii inafanya vyema.

Dawa wanayoifanyia utafiti inamchanganyiko wa mseto na dawa nyingine ili kupata mbadala na kuachana na SP kwa ajili ya kinga ya akina mama wajawazito na watoto ila tunamalizia utafiti ili tuje tutoe matokeo ifikapo machi mwaka huu.

Kwa upade wake Mtafiti wa Malaria wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilichopo Bombo Hospitali, Tanga, Deus Ishengoma ameiomba serikali kuwasaidia watafiti ili waweze kuibua tafiti zinazotoa majibu tofauti kwa jamii ambapo ka sasa ambapo tafiti nyingi zimekuwa zikigharimiwa na mashirika ya nje jambo linalowanyima uhuru kwa kufanya tafiti za kigunduzi.

"Serikali iliahidi kutoa asilimia moja ya pato la Taifa ili kuwawezesha watafiti nchi nzima ili waibue tafiti za kigunduzi, lakini mpaka leo kimya... tambueni fedha tunazopewa na mashirika ya nje zinakuwa zimelenga kile wanachokitaka wao na tufanye tofauti na tungewezeshwa kufanya tafiti za kigunduzi zingeleta tija kwa jamii, mfano kubuni mbinu mpya za kukabili Ugonjwa wa Malaria katika maeneo yenye Malaria kubwa kule Kanda ya Ziwa, Kigoma na Kusini mbinu ziwe tofauti, vile vile maeneo yenye maambukizi kidogo kama Dodoma, Kilimanjaro, Arusha na  Manyara na kuelekea ukanda wa nyanda za juu kusini mwa Tanzania napo kukawa na mbinu tofauti," Amesema Ishengoma.

Pia ameomba jamii kutumia vema vyandarua wanavyopewa ili kuzuia wasiumwe na mbu na kuachana na mila potofu zinazoweza kudhoofisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria ikiwemo kusema kuwa vyandarua vinazalisha kunguni, vinapoteza hamu ya unyumba kwa wapenzi na wengine wanafugua kuku.

Awali akifungua kongamano la Kisanyansi la Kitafiti ambapo Mada ilikuwa ni Mchango wa Chuo Kikuu MUHAS katika mapambano dhidi ya Malaria Tanzania lililofanyika jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, Prof Andrew Barnabas Pembe amewaomba watafiti kujitokeza kwa wingi kufanya tafiti zitakazoleta matokeo Chanya katika jamii yetu.

"Niwaombe watafiti wote kujitokeza kwa wingi kuungana na Chuo chetu Cha MUHAS ili tufanye  tafiti zenye tija ili kuweza kutatua matatizo mbali mbali kwa jamii," amesema.

Kongamano hilo la pili limehudhuriwa na watalaamu kutoka Wizara ya Afya, Shirika la Afya Duniani (WHO), SIDA Tanzania, Kituo cha Utafiti Ifakara, Mradi wa Taifa wa kuzuia Malaria pamoja na Vyuo mbali mbali na wadau wa Afya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post