WEMA SEPETU NA DIAMOND PLATNUMZ USO KWA USO.. WAZUA GUMZO LA AINA YAKE


Msanii wa Bongo Fleva, Wema Sepetu na Diamond Platnumz leo Alhamisi Januari 31, 2019 wamekuwa kivutio katika viwanja vya Leaders Club ambako mkutano kati ya wasanii na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda umefanyika.

Diamond amewasili viwanja hivyo majira ya saa 9:15 alasiri akiwa katika gari jeusi aina ya BMW X6 huku akiwa amevalia kanzu nyeupe na kilemba.

Akiwa amesindikizwa na walinzi wake, Diamond alipofika alielekea kushoto mwa jukwaa na kusalimia baadhi ya wasanii kabla ya kuelekea jukwaa kuu ambapo Wema na wasanii wengine walikuwa wamekaa.

Alianza kumsalimia ofisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara , meneja wake Babu Tale na kisha kumkumbatia mrembo huyo kwa takribani dakika moja kabla hajaenda kusalimia wasanii wengine akiwemo King Kikii, Masanja Mkandamizaji na wengine.

Tukio hilo lilionekana kuwavutia watu waliofika katika viwanja hivyo wakiwemo waandishi wa habari ambao kila mmoja alikuwa akipambana kupata picha.

Na Nasra Abdallah na Hellen Hartley, Mwananchi 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527