Wednesday, January 23, 2019

RAIS MAGUFULI AAMBIWA ANATISHA, SIYO RAHISI MTU KUROPOKA MBELE YAKE

  Malunde       Wednesday, January 23, 2019

Mwenyekiti wa Wanawake wa Wakiislam Mkoa wa Dar es Salaam, Pili Abdallah amewaomba mawaziri kuwa na mazoea ya kukutana na viongozi wa dini ili kuwa na uhuru wa kuwaeleza masuala mengi ya kitaifa.

Wito huo ameutoa leo Jumatano Januari 23, 2019 kwenye mkutano maalumu na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini kati yao na Rais Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Pili amesema kuna masuala ambayo hayafai kuzungumza moja kwa moja na Rais, hivyo itakuwa rahisi kuyazungumza wakikutana na mawaziri.

”Rais naomba mawaziri nao waonane na viongozi wa dini kwa wakati wao kama ulivyokutana hivi, mawaziri wakiita vikao kama hivi tutaweza kusema mengi kwa sababu baba (Rais Magufuli) unatisha, siyo rahisi mtu kuropokaropoka, tunaweza tukawa na mengi lakini tukayafichaficha,” amesema mama huyo na kuongeza:

“Hata mimi nina mengi lakini kama ningempata waziri husika, tuko naye tungeweza kuongea mengi na ungefikishiwa mengi ya kutupeleka mbele.” 


Na Emmanuel Mtengwa, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post