WANAFUNZI WALIOFAULU KIDATO CHA KWANZA LAKINI HAWAJUI KUSOMA, KUANDIKA KUCHUNGUZWA

Halmashauri ya wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya inakusudia kufanya uchunguzi juu ya madai ya kuwapo kwa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu licha ya kuwa hawajui kusoma wala kuandika.

Madai hayo yameibuliwa na diwani wa Rujewa, Mkude Msasi katika kikao cha baraza hilo kilichofanyika leo katika ofisi za maji bonde la Rufiji wilayani humo.

Msasi amedai wapo wanafunzi wengi waliofaulu pasi kujua kusoma wala kuandika huku akieleza anao ushahidi wa wanafunzi hao.

"Mimi shuleni kwangu nina wanafunzi 536 lakini kuna wanafunzi zaidi ya mia na kitu hawajui kusoma wamechaguliwa wako pale," amesema Msasi.


Na Yonathan Kossam, mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527