Thomas Absalom (aliyeshikilia Mwenge)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa wakuu wawili wa Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga na Mkuu wa Wilaya ya Tarime.
Nafasi ya Mkuu wa wilaya ya Mwanga, ameteuliwa Thomas Absalom na Mkuu wa Wilaya ya Tarime ameteuliwa ndugu Charles Kabeho.
Ndugu Charles Kabeho alikuwa kiongozi wa mwenge mwaka 2018 ambao ulizunguka nchi nzima kukagua na kuzindua miradi mbalimbali.
Pia Rais John Magufuli amewateua majaji 6 wa Mahakama Kuu, kuwa majaji wa Mahakama ya Rufani na mahakimu na wanasheria 15 kuwa majaji wa Mahakama Kuu.
Wateuliwa wote wataapishwa Jumanne, 29 Januari, Ikulu Jijini Dar es salaam.