MSANII WA FILAMU AFARIKI DUNIA


 Kader Khan enzi za uhai wake.

Msanii Mkongwe wa Filamu kutoka kisima cha Bollywood, Kader Khan, amefariki dunia hapo jana akiwa nchini Canada alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kader ambaye pia alikuwa mtunzi wa filamu na script, amefariki dunia hii leo kwa saa za India akiwa na miaka 81, baada ya kupata maradhi yanayotokana na kuwa na umri mkubwa, ikiwemo matatizo ya mfumo wa chakula.

Kifo cha Khan kimegusa wasanii mbali mbali wa filamu India akiwemo muigizaji mkongwe, Amitah Batchan, ambaye ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter.
Wakati wa uhai wake Khan ameshiriki filamu zaidi ya 300 za Bollywood, ambazo zimempa heshima kubwa kwenye tasnia ya filamu nchini India na duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post