DC KISHAPU ASIMULIA JINSI ALIVYONUSURIKA KIFO WAKATI WA KUJIFUNGUA

Mkuu  wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba alisema jukumu la kuzuia vifo kwa watoto wachanga na kinamama wajawazito linagusa sekta zote, kwasababu ya changamoto mbalimbali zinazotajwa kusababisha vifo hivo ikiwemo ya ukosefu na upungufu wa miundombinu ya huduma za afya katika vituo vya afya. 



 Talaba ameeleza changamoto za uzazi alizopitia wakati akitoa shuhuda kwenye kikao cha wadau wa afya, na kusema yeye ni miongoni mwa wanawake waliopitia adha hizo. 

Amesema alikuwa akijifungua watoto wakubwa mwenye uzito wa kilo tano na kwamba alinusurika kupoteza maisha endapo asingepata huduma bora kutoka kwa wataalamu wa afya. 

“Mimi nimepitia matatizo ya uzazi kwasababu nilikuwa najifungua watoto wakubwa wenye kilo tano,kwa hiyo haikuwa kazi ndogo pengine nisinge zalia hospitali nzuri ningepoteza maisha,” alisema Talaba. 

“Ni wajibu wa kila mwanajamii kusimamia nafasi yake katika kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa kuhakikisha anatatua changamoto za kimiundombinu, na kutoa elimu sahihi ya sehemu husika ya kupata huduma bora za afya,” aliongeza Talaba. 

Mkoa wa Shinyanga leo Januari 18,2019 umezindua kampeni ya uwajibikaji katika kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi ijulikanayo kwa jina la JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA yenye lengo la kuzuia na kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga.

Na Malaki Philipo - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527