Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS)

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano  nchini (TCRA), Injinia James Kilaba, amesema Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) utasaidia kurahishisha usimamiaji wa masuala mengi hasa katika ukusanyaji wa mapato hivyo kuiongezea nchi nafasi ya kukua kiuchumi.


Ameyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa kuhusu mfumo huo katika makabidhiano ya yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 18.

Injinia Kilaba amesema TCRA inafanya kazi kwa ukaribu na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), ambapo mfumo huo utawasaidia kukusanya taarifa muhimu za wateja wao kwa kutumia njia ya simu.

“Mfumo huu una faida sana katika nchi yetu lakini hasa katika ukusanyaji wa mapato kwa sababu utawezesha kutambua vyanzo vya mapato ya watoa wa huduma za fedha kwa njia ya simu na itawasaidia TRA kufanya kazi zao kwa urahisi,” amesema.

Amezitaja faida zingine zitakazopatikana kutokana na mfumo huo utawezesha kupatikana takwimu za mawasiliano yanayofanyika ndani na nje ya nchi, kupata na kugundua mawasiliano ya simu za ulaghai na kutambua ada za huduma za fedha mtandaoni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527