WALIOTUHUMIWA KULIPUA BOMU WALIPWA MAMILIONI YA FEDHA


Raia watatu waliotuhumiwa kuhusika na mlipuko wa bomu nchini Uganda mwaka 2010, wamezawadiwa kiasi cha shilingi milioni 8 ambazo ni sawa na milioni 181 na Mahakama Kuu Jijini Nairobi nchini Kenya.

Raia hao waliojulikana kwa majina ya Mohamed Adan Abdow, Mohamed Hamid Suleyman na Yahya Suleyman wamelipwa fedha hizo kwa ajili ya fidia juu ya ukiukwaji wa uhuru na haki zao za msingi waliofanyiwa.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu, David Majanja amesema kuwa kukamatwa kwa kukamatwa na kuondolewa kwa raia hao kutoka Kenya hadi nchini Uganda kulikuwa ni kinyume cha sheria.

Mwaka 2010 watuhumiwa hao waliiomba Mahakama kupitia upya suala hilo la kukamatwa kwao na kuhamishiwa nchini Uganda wakisema kuwa halikufuata sheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post