MATANGAZO YA MICHEZO YA KUBAHATISHA YAZUIWA TANZANIA

Michezo ya kubatisha nchini Tanzania imekuwa maarufu huku washiriki zaidi wakiwa vijana lakini sasa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imezuia kwa muda urushaji wa matangazo ya michezo hiyo kupitia redio na televisheni.

Bodi hiyo imedai kuwa matangazo hayo yamekuwa mengi kiasi cha kuharibu taswira ya mchezo huo.

Taarifa ya bodi hiyo ya Januari 23, 2019 iliyosainiwa na kaimu mkurugenzi mkuu, James Mbalwe inaeleza kuwa hatua ya kusitisha matangazo hayo ni kutokana na malalamiko miongoni mwa wananchi juu ya kukithiri kwa matangazo kwenye vyombo hivyo vya habari.

“Kumekuwa na ongezeko la malalamiko kutoka kwa umma juu ya kukithiri kwa matangazo ya michezo ya kubahatisha hapa nchini,” inaeleza taarifa hiyo.

“Bodi imesitisha kwa muda urushaji wa matangazo ya michezo ya kubahatisha kupitia redio na televisheni. Matangazo yanayotolewa kupitia vyombo vingine hayaathiriwi na zuio hili.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post