Picha : DC MBONEKO AWATEMBELEA HOSPITALI WANAFUNZI WALIOPATA AJALI SHINYANGA

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko amefika katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajulia hali wanafunzi waliopata Ajali ya basi la Shule ya msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.    

Ajali hiyo imetokea leo Alhamis Januari 10,2019 majira ya saa tisa alasiri wakati basi hilo lenye namba za usajili T183 AFE likitoka shuleni eneo la Bugayambelele kata ya Kizumbi kuelekea Ushirika likirudisha wanafunzi majumbani.

Akiwa hospitalini hapo Bi. Mboneko amewaagiza madaktari na wauguzi wote waliokuwa wamemaliza muda wao wa kuwepo kazini kurudi mara moja kwa ajili ya kutoa huduma ya dharula kuwahudumia majeruhi hao.

“Kuna Watoto wengine naona wana tatizo la meno hivyo Madaktari waliotoka warudi kusaidia kuwahudumia watoto , hii dharura imetokea ni lazima ifanyike vizuri” alisema Mboneko.

Aidha Bi. Mboneko amewapongeza wauguzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa Wa Shinyanga kwa kutoa huduma ya haraka kwa majeruhi wa ajali hiyo huku akimsisitiza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dokta Harbet Masigati kusimamia vyema majeruhi waliobaki wamelazwa hospitalini hapo .

“Ila niwapongeze sana kwa namna mlivyojitolea kuwahudumia hawa watoto mmewahudumia vizuri na kwa haraka , naombeni muendelee hivyo hivyo kwa hawa waliobaki” alisema Mboneko

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dokta Herbet Masigati amesema wamepokea watoto 30 baada ya kuwahudumia na wengi wao wamewaruhu na kubaki na wanafunzi takribani wanne huku akiweka wazi kuwa hali zao zinaendelea vizuri.

Kwa Mujibu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule chanzo cha ajali hiyo ni dereva kuendesha gari huku akichezea simu/akichat huku akiongeza kuwa mara baada ya ajali kutokea dereva alikimbia.

SOMA ZAIDI <<HAPA>> RPC AZUNGUMZIA AJALI YA WANAFUNZI LITTLE TREASURES

ANGALIA PICHA 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko akiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwajulia hali wanafunzi waliopata Ajali ya basi la Shule ya msingi Little Treasures iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga.Picha zote na Steve Kanyefu Malunde1 blog

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dokta Herbet Masigati (kushoto) amesema wamepokea watoto 30 baada ya kuwahudumia na wengi wao wamewaruhu na kubaki na wanafunzi takribani wanne huku akiweka wazi kuwa hali zao zinaendelea vizuri.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwajulia hali baadhi ya wanafunzi waliopata ajali ya bali la Shule ya msingi Little Treasures


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akishirikiana na Wahudumu wa Afya kutoa huduma kwa majeruhi



Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga akitoa huduma kwa mtoto mwenye majeraha yaliyotokana na ajali

Huduma zikiendelea kutolewa kwa majeruhi

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi waliopata ajali wakiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga

Basi la shule ya Little Treasures 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527