KOCHA MKUU WA YANGA AREJEA DAR


Mwinyi Zahera

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Mwinyi Zahera amerejea nchini usiku wa kuamkia leo Desemba 27,2018, ambapo mara tu baada ya kufika amesema programu zote za maandalizi ya mechi dhidi ya Mbeya City anaziacha kwa kocha msaidizi Noel Mwandila.

Akiongea mara baada ya kutua uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akitokea Ufaransa, Zahera amesema kuelekea mechi hiyo hataingilia chochote kwenye maandalizi kwani kocha msaidizi ameshamalizana na wachezaji.

''Kwasababu wachezaji wamefanya program zote za mechi timu nitaiacha kwa Noel aendelee na mchezo huu ambao najua wachezaji wanajua umuhimu wake kwetu'', amesema Zahera.

Zahera ambaye alikwenda nchini Ufaransa kushughulikia masuala yake binafsi ya kibiashara ameongeza kuwa lengo lake ni kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa wanaongoza ligi na wachezaji wanalijua hilo.

Yanga ambayo inaongoza ligi, itakuwa ugenini Desemba 29, 2018 kukipiga na Mbeya City katika mchezo wa raundi ya 18 kabla ya kurejea Dar es salaam kucheza na Azam FC na kukamilisha michezo 19 ya mzunguko wa kwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post