WAMBURA AANIKA SABABU ZA KUIBURUZA TFF MAHAKAMANI


Michael Wambura ambaye ameshinda kesi yake hivi karibuni dhidi ya kupinga kuondolewa na TFF katika nafasi yake, amesema kuwa alichukua uamuzi wa kuiburuza mahakamani baada ya kutojibiwa barua yake alipoliomba shirikisho hilo kukaa mezani na kumaliza matatizo yao.


"Kabla ya kwenda Mahakamani niliwaandikia TFF barua kuwaomba tukutane kwaajili ya usuluhishi, lakini hawakujibu ndio maana nikaenda mahakamani," amesema.

"Nimekwenda mahakamani sio kwa kuishtaki TFF lakini nimeenda kutafuta haki juu ya maamuzi yaliyofanyika na kamati za TFF jambo ambalo ni kawaida na wala halijaanza leo," ameongeza.

Pia Wambura amezungumzia juu ya mkanganyiko uliopo juu ya uhalali wake wa kulipeleka suala hilo katika Mahakama za kiraia, ambapo amesema, "katiba ya FIFA pamoja na ya TFF zinaeleza wazi kuwa mashirikisho haya yote hayapo juu ya sheria".

Michael Wambura alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa TFF, Agosti 12, 2017 kabla ya kufungiwa maisha kutojihusisha na soka Machi 15, 2018. Na mwezi Novemba 30, mwaka huu Mahakama imemrejesha madarakani.

Chanzo:Eatv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527