UVCCM WAMPITISHA MAGUFULI KUGOMBEA URAIS 2020

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, kupitia kwa Katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi Hassan Bomboko, imesema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020 umoja huo utaenda Dodoma kuhakikisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa sasa Rais John Pombe Magufuli, anapewa nafasi ya kuwania tena Urais.
Kwa mujibu wa Bomboko kwenye kikao kitakachofanyka Dodoma Umoja huo hautakuwa na lengo jingine zaidi ya kumpitisha Rais Magufuli kuwania tena nafasi hiyo ya kukiongoza chama hicho kwenye uchaguzi wa awamu ya pili.

"Kama msemaji rasmi wa UVCCM, msimamo wa taasisi yetu ni kwamba hatuna na hatutakuwa na mchakato wa kumtafuta mgombea Urais 2020 mwingine zaidi ya Magufuli ambaye ndiyo Mwenyekiti wa CCM" amesema Hassan Bomboko, UVCCM.

Aidha Bomboko amesema kuwa "mwaka 2020 tutakwenda Dodoma kwenye mchakato wa kidemokrasia Kukamilisha desturi yetu ya CCM ya kumbariki mgombea wetu kwa muhula wa pili, uchaguzi wa mgombea wa CCM tulishamaliza mwaka 2015"

"Kwa wenye nia ya kugombea Urais 2020 kupitia CCM watafute biashara nyingine ya kufanya kwani CCM hakuna Urais wa kupeana kiushemeji" ameongeza Hassan Bomboko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post