Tanzia : MWANASIASA MKONGWE PANCRAS NDEJEMBI AFARIKI DUNIA


Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Pancras Ndejembi amefariki dunia leo Jumamosi Desemba 29, 2018 majira ya saa 3:30 asubuhi.

Ndejembi amefariki katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikopelekwa jana Ijumaa baada ya hali yake kubadilika ghafla.

Mtoto wa Marehemu, Edna Ndejembi amesema baba yake alikuwa anasumbuliwa na kifua kubana ambapo alilazwa katika Hospitali ya DCMC ya jijini Dodoma na kuruhusiwa juzi Alhamisi akiwa ameimarika kiafya.

"Lakini jana jioni hali yake ilibadilika ghafla ndipo tukamkimbiza hapo hospitali ya mkoa na leo saa tatu asubuhi mzee ametutoka," amesema Edna.

Mzee Ndejembi aliwahi kuwa mkuu wa wilaya katika wilaya mbalimbali nchini na baadaye akawa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma na mwenyekiti wa wenyeviti wa mikoa kwa miaka 20.

Pia, ni miongoni mwa waliokuwa mawaziri katika utawala wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post