TUMEKUSOGEZEA TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA JUMANNE DEC 18, 2018, JUVENTUS WAMNYEMELEA POGBA

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsaini kiungo mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Uhispania Isco, 26, baada ya msimu kukamilika. Tayari mazungumzo ya awali kati ya miamba hao wa England na mchezaji huyo yameshafanyika. (As - in Spanish)

Manchester United itawapasa kutoa kitita cha pauni milioni 24 kama wataamua kumfuta kazi kocha wao Jose Mourinho kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi Januari. (Daily Record)

Kiungo wa zamani wa Liverpool Danny Murphy amesema muda wa kumfuta kazi Mourinho ni huu. (Talksport)

Wakuu wa ligi ya Premia wanataka kufanya mazungumzo na wachezaji weusi ili kutafuta njia bora za kupambana na ubaguzi mchezoni - wachezaji weusi wanatazamiwa kuvigomea vyombo vya habari kama sehemu ya mapambano dhidi ya ubaguzi. (Mirror)

Klabu ya Chelsea inajipanga kuwafungia mashabiki wanaofanya ghasia nje ya uwanja wao wa Stamford Bridge kutohudhuria mechi za klabu hiyo. Hivi majuzi, klabu hiyo imewafungia kwa muda kupisha uchunguzi mashabiki wake wanaodaiwa kumtolea shutuma za kibaguzi nyota wa Manchester City, Raheem Sterling. (The Times)

Klabu ya Juventus imekutana na wakala Mino Raiola kuzungumzia uhamisho wa mchezaji nyota Paul Pogba wa Manchester United. Pia mazungumzo hayo yamehusisha usajili wa mlinzi kinda wa Ajax Matthijs de Ligtmet mwenye miaka 19 na kuongeza mkataba wa mshambuliaji kinda wa Italia mwenye miaka 18 Moise Kean. (Sky Italia via Football Italia)Paul Pogba, alisajiliwa na Manchester United kwa kima cha pauni Milioni 89 akitokea Juventus

Vigogo hao wa Italia wanataka kumrejesha Pogba jijini Turin baada ya kubaini kuwa United wanataka kumuuza katika dirisha la usajili la mwezi Januari. (Tuttosport via Mirror)

Beki raia wa Ujerumani anayekipiga katika klabu ya Chelsea Antonio Rudiger, 25, amesema bado hajaongea na uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake jijini London kuhusu kuongeza muda wa kandarasi yake. (Metro)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post