TETESI ZA SOKA BARANI ULAYA JUMATATU DEC 17

Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane amesema haitakuwa jambo gumu kwa kiungo Paul Pogba kuuzwa baada ya kukamilika kwa msimu baada ya nyota huyo kuwekwa benchi wakati United ikipokea kichapo kutoka kwa Liverpool hapo jana katika uga wa Anfield. (Sky Sports)

Klabu ya Everton imejitosa katika mbio za kumsajili beki kisiki wa West Ham Reece Oxford, 20. (Mail)

Klabu ya Barcelona wameorodhesha listi ya washambuliaji saba katika harakati za kumsajili mrithi wa mshambuliaji mkongwe Luis Suarez. (Mundo Deportivo via Mirror)
Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 16.12.2018
Baba wa nahodha wa Stuttgart afariki uwanjani baada ya mechi

Kipa nyota wa zamani wa Real Madrid Iker Casillas amemkosoa vikali bosi wa Manchester United Jose Mourinho baada ya timu hiyo kupokea kichapo cha 3-1 mbele ya Liverpool akiuliza: "Ni wakati gani unaona kuwa makocha hawafai kuongoza timu au treni?" (Mirror)
Klabu kadhaa za England zinamfuatilia mshambuliaji mwenye miaka 21 aliyezaliwa jijini London Ronald Sobowale - ambaye ni binamu wa nyota wa Bayern Munich David Alaba. Sobowale kwa sasa anacheza mpira wa ridhaa nchin England. (Mail)

Bosi wa Cardiff City Neil Warnock amesema atajitahidi kuboresha kikosi chake "kwa nafasi mbili au tatu" itakapofika January. (Sky Sports)


Kocha wa Bournemouth Eddie Howe amesema bado anaangalia uwezekano wa kuboresha kikosi chake katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari. Hata hivyo, amesema hana hakika kama watapata wachezaji bora kuliko wale ambao wanao kwa sasa. (Bournemouth Daily Echo)
Tetesi bora za Jumapili

Meneja wa United Jose Mourinho anasema hajui ikiwa klabu hiyo inamuunga mkono kwa ajili ya usajili wa wachezaji kwenye dirisha la usajili la majira ya joto la mwezi ujao wa Januari. (Observer)

Arsenal wanamtaka mchezaji wa Boca Juniors mwenye miaka 22 raia wa Argentina Cristian Pavon - lakini atagharimu dola milioni 40. (Sun on Sunday)Mlinda mlango Keylor Navas kusalia Santiago Bernabeu

Kipa wa Costa Rica Keylor Navas, 32, hataondoka Real Madrid Mwezi Januari. (Marca)

Mshambuliaji wa Inter Milan raia wa Argentina Mauro Icardi, 25, anasema mazungumzo bado yanaendea na klabu kuhusu kuongezwa mkataba wake. (Goal)

Kocha wa PSV Eindhoven coach Mark van Bommel amezungumza na kiungo wa kati Arjen Robben kuhusu kurudi kwenye klabu. Robben ataondoka Bayern Munich mwisho wa msimu. (Bild - in German)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post