SERIKALI YASITISHA AJIRA ZA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII


Serikali imesema imesitisha kuajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii kupitia mradi wa Global Fund na badala yake inaelekeza nguvu kuajiri watumishi kwenye sekta ya afya.


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege alisema hayo baada ya kuwapo kwa barua inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayotoka Tamisemi ikielekezwa kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mbeya na Chunya, ikimtaka kusitisha ajira hizo.


Kandege alisema Wizara ya Afya inajenga vituo vya afya na zahanati nyingi vijijini na mijini, hivyo ina uhitaji mkubwa wa wahudumu wa afya.


“Tukiwaajiri wahudumu wa afya ngazi ya jamii huku zahanati na vituo vya afya tulivyojenga vina ubora na uwezo wa kutoa huduma kubwa ikiwamo upasuaji, ina maana tulichofanya itakuwa kazi bure,” alisema

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chunya mkoani Mbeya, Sophia Kumbuli alisema kulikuwa na mchakato unaendelea wa kutaka kuajiri watu wa kada hiyo, lakini suala la kusitishwa hana taarifa nalo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post