TAASISI YA GOVERNANCE LINKS YAKABIDHI MIRADI YA MFANO JIJINI MWANZA


Mkurugenzi wa taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania, Donald Kasongi (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu Mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) wakati wa zoezi la kukabidhi matenki ya kuvuna maji ya mvua yaliyojengwa kupitia mradi huo katika Shule za Msingi Mabatini A na B zote za Jijini Mwanza, hii leo Disemba 21, 2018.

Mradi wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) ulibuniwa na taasisi ya Governance Links Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Mwanza ukilenga kuwajengea uwezo wananchi pamoja na wadau/ taasisi mbalimbali kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na hatari ya Majanga ikiwemo mafuriko.
Mkurugenzi wa taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania, Donald Kasongi amesema ujenzi wa matenki ya mfano ya kuvuna maji ya mvua katika Shule za Msingi Mabatini A na B Jijini Mwanza, umegharibu shilingi Milioni tano hivyo wananchi na Shule nyingine zinaweza kutumia mradi huo kujifunza namna bora ya kuvuna maji ya mvua badala ya kupoteza kiasi kikubwa wakati wa mvua.
Utekelezaji wa Mradi wa majaribio wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) ulianza mwezi Otoba 2017 na unafikia tamati mwezi huu Disemba 2018 huku kukiwa na matarajio makubwa ya mradi huo kuwa endelevu.
Taasisi ya Maendeleo na Utafiti ya Governance Links Tanzania imekabidhi manteki mawili ya kuvuna maji ya mvua katika Shule za Msingi Mabatini A na B, yaliyojengwa kupitia mradi wa Ustahimilivu katika Jijini la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience). 

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Donald Kasongi amesema ujenzi wa matenki hayo ya mfano umegharimu shilingi Milioni tano hivyo wananchi na Shule nyingine Jijini Mwanza zinaweza kutumia mradi huo kujifunza namna bora ya kuvuna maji ya mvua badala ya kupoteza kiasi kikubwa cha maji wakati wa mvua. 

Kasongi amesema hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Ustahimilifu katika Jiji la Mwanza (Mwanza Environmental Governance Partinaship for Resilience) unaolenga kuwajengea uwezo wananchi pamoja na wadau/ taasisi mbalimbali kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi pamoja na hatari ya Majanga ikiwemo mafuriko. 

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, wanafunzi Mariam Thomas (Mabatini B), Rayton Mandalu (Mabatini A) pamoja na Rhoda Madaraka (Mabatini B) wamesema uvunaji wa maji ya mvua umewasaidia kupata maji ya kutosha kwa ajili ya usafi wa madarasa, vyoo, kumwagilia miche ya miti na hivyo kuwaondolea adha iliyokuwepo awali.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527