Picha : WATOTO NA VIJANA WA ARIEL CAMP 2018 WAKICHEZA MICHEZO MBALIMBALI BEACH DAR

Watoto na vijana kutoka mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Simiyu na Mara wanaoshiriki katika Kambi ya Ariel 2018 inayofanyika jijini Dar es salaam wameendelea kufurahia kambi kwa kucheza michezo mbalimbali katika Beach ya Serene jijini Dar es salaam.

Kambi ya Ariel 2018 iliyoanza Desemba 10,2018 inashirikisha watoto na vijana 50 ambao ni wanachama wa klabu za vijana na watoto zinazosimamiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) inayolenga kutokomeza VVU na UKIMWI kwa watoto na familia.

Angalia picha hapa chini
Vijana wakiwa pozi.

Watoto wakiruka sarakasi.

Vijana wakicheza mchezo wa sarakasi.
Watoto wakiruka kamba.
Mchezo wa mpira wa nyavu ukiendelea.
Vijana warukasi sarakasi kutoka taasisi ya Babawatoto wakitoa burudani kwa watoto na vijana wa Kambi ya Ariel 2018.
Burudani ya sarakasi ikiendelea.
Michezo inaendelea.
Mbio za magunia zikiendelea.
Mchezo wa kuvuta kamba ukiendelea.
Watoto na vijana wakiwa ndani ya Swimming pool wakifurahia wakati wakiogelea katika Beach ya Serene Hotel.
Picha katika ufukwe wa Bahari ya Hindi.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527