MWASITI AFUNGUKA JUU YA MAHUSIANO YAKE ASEMA KWA UMRI WAKE KUWA SINGLE NI UONGO

Msanii wa kike katika kiwanda cha Bongo Fleva, Mwasiti amesema kuwa kwa sasa hawezi tena kudanganya katika 'interview' kuwa yuko single kama zamani kwasbabu ya umri wake.

Mwasiti amesema kuwa wanamuziki wengi wa kike hasa miaka ya nyuma walikuwa wanaogopa kusema ukweli kuwa wana mahusiano kwa kuhofia kuwa wataonekana tofauti na wengine wakihofia kutopata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wanaume, lakini kwa sasa ni tofauti na sio jambo la ajabu kwa mwanamuziki wa kike kumtaja mpenzi wake.

"Niko kwenye mahusiano, niko kwenye mahusiano mazuri tu na nina furaha, kwa umri niliofikia kila siku kwenda kwenye 'Interview' na kusema niko single ni uongo, ina maana hata hufuatwi na wanaume?," amesema Mwasiti.

Pia amezungumzia kazi yake mpya aliyomshirikisha Roma inayojulikana kama 'Fall in love' kuwa imekwenda vizuri kutokana na Roma kutaka uhalisia zaidi katika video, ndiyo maana katika 'scene' nyingi wameonekana kama ni wapenzi.

"Sehemu nyingi mnazoziona sio kama tulikuwa tunaigiza, tukicheka tunacheka kweli, ilikuwa nzuri kwasababu Roma alikuwa anataka uhalisia kwenye video. Alikuwa anataka watu waache zile kwamba wewe mume wa mtu unafanya Bongo Fleva basi huwezi kufanya kazi na mwanamuziki wa kike na mkafanya vitu ambavyo wanafanya wapenzi," ameongeza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post