MTOTO AZALIWA KUTOKA TUMBO LA UZAZI LA MTU ALIYEKUFA

Mtoto mwenye afya aliyezaliwa baada ya upandikizaji kutoka kwa mtu aliyekufa


Mtoto wa kike mwenye afya amezaliwa kutokana na kupandikiza tumbo la uzazi kutoka kwa mwili wa mtu aliyekufa.

Upasuaji uliofanyika kwa saa kumi, ulifanyika mjini São Paolo, Brazil, mwaka 2016.

Mama mwenye umri wa miaka 32 alizaliwa bila kuwa na tumbo la uzazi.

Kumekuwa na upandikizaji wa matumbo 39 ya uzazi kwa kutumia wachangiaji walio hai, wakiwemo wazazi wanaojitolea matumbo yao kwa mabinti zao na kufanya kuzaliwa kwa watoto 11.

lakini majaribio kumi ya upandikizaji kutoka kwa matumbo ya watu waliokufa hayakufanikiwa au wakati mwingine mimba zilitoka

Katika hatua hii mpya, aliyejitolea tumbo la uzazi ni mama wa umri wa miaka ya 40 mwenye watoto watatu ambaye alipoteza maisha baada ya kuvuja damu kwenye ubongo.

Chanzo:Bbc

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527