MWALIMU ALIYEPOKEA MISHAHARA MIWILI 2012 HADI 2015 ATUPWA JELA MASWA


Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imemhukumu kifungo cha miaka mitatu jela pamoja na kurejesha Sh milioni 10.3, Mwalimu Josiah Mkome baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa inamkabili.

Mwalimu Mkome alikuwa akifundisha Shule ya Sekondari Kandawe wilayani Magu, mkoani Mwanza alishtakiwa kwa kosa la kupokea mishahara miwili kutoka katika Wilaya ya Magu na Maswa kinyume cha sheria.

Mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa, amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Fredrick Lukuna, mshtakiwa alipokea mishahara hiyo miwili kiasi ya hicho cha
Tangu Februari mwaka 2012 hadi Mei mwaka 2015.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527