MBOWE ATUMA UJUMBE AKIWA GEREZANI

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, amewataka wafuasi wake wasihuzunike na hatua ya yeye kuwekwa rumande kwa madai ya kutopatiwa dhamana bali watumie nafasi hiyo kuombea tume huru ya uchaguzi.

Kauli hiyo ya Mbowe imetolewa Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho bara na mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya kusikilizwa rufaa ya kupata au kutopata dhamana kwa viongozi hao wawili.

"Mwenyekiti amesisitiza sana, kutomlilia yeye bali walilie taifa letu kutafuta mabadiliko, kudai tume huru ya uchaguzi, kwa sababu kesi hii msingi wake ni uchaguzi uliosababisha kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina kwa hiyo naomba wajitokeze kwa waingi kesho," amesema Mnyika.

Wakati huohuo Mnyika amebainisha kuwa chama hicho kupitia mawakili wake kimewasilisha maombi ya kuiomba mahakama kutoa kipaumbele kwa kesi dhdi ya viongozi wake kabla ya mahakama hiyo haijaenda likizo.

Mbowe na Matiko wako mahabusu baada ya kufutiwa dhamana kwenye kesi yao ya msingi inayowakabili juu ya kusababisha kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa NIT, Akwilina Akwilini ambapo walifutiwa dhamana hiyo kwa madai ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527