AMUUA KAKAAKE WAKITIBIWA KWA MGANGA WA JADI

Watu wawili wamefariki dunia Mkoani Morogoro baada ya mtu aliyedaiwa kuwa na ugonjwa wa akili kumuua ndugu yake na kisha yeye mwenyewe kujinyonga walipokuwa kwa mganga wa kienyeji kwaajili ya kupata matibabu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Wilbord Mtafungwa amesema kuwa tukio hilo limetokea desemba 1, 2018 baada ya Lucian Kigolo (54) ambaye anamatatizo ya akili kumshambulia kaka yake Gerald Kigolo(60) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.


Aidha Kamanda huyo amesema baada ya kutenda tukio hilo, mtu huyo aliamua kujinyonga kwa kutumia kamba nyumbani kwa mganga wa kienyeji ambaye ametambulika kwa jina la Luka Paulo (50), ambapo katika tukio hilo Jeshi la Polisi linamshikilia mganga huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527