WANAUME GEITA WALALAMIKIWA KUINGILIA WAKE ZAO KWA NGUVU


Picha haihusiani na tukio.

Wanaume mkoani Geita wamedaiwa kuwa chanzo cha migogoro ndani ya familia zao kutokana na tabia ya kuwaingilia kwa nguvu wenza wao wakati wanapohitaji tendo la ndoa pasipo kujali kufanya hivyo ni kutenda jinai.

Hayo yameelezwa na baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wilaya uliokuwa ukitathimini mikakati ya kupambana na ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na shirika la IRS uliomalizika, ambapo wamedai jambo hilo husababisha ongezeko la migogoro mingi kwenye ndoa inayopelekea watu kuuana na hata kupeana vilema vya kudumu.

Washiriki hao wamesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wanaume kuwaingilia kinguvu wake zao wakati wakihitaji tendo la ndoa pasipo hata kuwaandaa, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya makosa ya kujamiiana lakini pia linahatarisha ustawi wa ndoa husika.

Naye, Wakili wa Serikali Janeth Kisibo, amedai matatizo hayo yanasababishwa kutokaa na ukosefu wa elimu ya kujua namna gani wanandoa wanapaswa kuishi. Jambo ambalo linasababisha ukatili wa kijinsia kuwa mkubwa na makosa mengine yanayopelekea vifo na ubakaji.

Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post