MAKONDA AANZA KUSHUGHULIKA NA MABUSHA


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana Desemba, 15, 2018, amezindua kampeni ya utoaji wa kinga ya Matende, Minyoo, Mabusha na Kichocho kwa wa wakazi wa mkoa huo.

Katika uzinduzi huo Mh. Makonda amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupata kinga ili kujiepusha na magonjwa hayo.

''Ndugu zangu niwaombe tujitokeze kupata kinga hii, maana itatolewa kwenye vituo zaidi ya 923 ikiwemo Vituo vya afya, Mashuleni, Ofisi za watendaji Kata na mitaa, Vituo vya mabasi na Sokoni lengo ni kuwafikia wananchi wote'', amesema.

Mkuu huyo wa mkoa ameeleza kuwa kama mkoa wamekusudia kuwafikia zaidi ya wananchi 5,600,000 sawa na 100% ya wananchi wenye uhitaji wa kupatiwa kinga hiyo katika mkoa wa Dar es salaam.

Aidha Makonda ameipongeza Sekta ya afya kwa kazi kubwa wanayoifanya katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post